Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Riches

225 mistari · 107 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;

  2. Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi.

  3. wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?

  4. Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.

  5. Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha,

  6. ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.

  7. Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.

  8. “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

  9. Usitumainie vya udhalimu wala usijivune kwa vitu vya wizi; ingawa utajiri wako utaongezeka, usiviwekee moyo wako.

  10. Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.

  11. Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.

  12. Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni.

  13. Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.

  14. Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.

  15. Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.

  16. Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho.

  17. Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

  18. Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki.

  19. Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.

  20. Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu.

  21. Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

  22. Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.

  23. Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

  24. Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.

  25. Mtu maskini huomba kuhurumiwa bali tajiri hujibu kwa ukali.