Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Repentance

343 mistari · 65 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo,

  2. msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya kule Meriba, kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani,

  3. kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.

  4. Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”

  5. Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake.

  6. Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.

  7. “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa?

  8. Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu.

  9. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu,

  10. kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

  11. mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  12. wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

  13. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.

  14. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,

  15. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  16. watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.

  17. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.

  18. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”

  19. Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.

  20. Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.

  21. Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.

  22. jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu! Acheni kutenda mabaya,

  23. jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

  24. Mabaki watarudi, mabaki wa Yakobo watamrudia Mungu Mwenye Nguvu.

  25. Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliwaita siku ile ili kulia na kuomboleza, kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia.