Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Repentance: Exhortation to

21 mistari · 65 vipengele

Mistari kuhusu Exhortation to

  1. Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu.

  2. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu,

  3. kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

  4. mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  5. wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

  6. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.

  7. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,

  8. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  9. watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.

  10. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.

  11. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”

  12. Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa.

  13. Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake,

  14. Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.

  15. Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako!

  16. Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana. Mwambieni: “Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali.

  17. Ashuru hawezi kutuokoa, hatutapanda farasi wa vita. Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’ kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza, kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”

  18. Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi;

  19. msitafute Betheli, msiende Gilgali, msisafiri kwenda Beer-Sheba. Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni, na Betheli itafanywa kuwa si kitu.”

  20. Mtafuteni Bwana mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima.

  21. “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”