Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Birds

71 mistari · 107 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,

  2. bundi, mumbi, bundi mkubwa,

  3. mwari, nderi, mnandi,

  4. korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

  5. Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

  6. Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

  7. Kama ukikuta kiota cha ndege kando ya barabara, iwe juu ya mti au chini, naye ndege amelala juu ya makinda au mayai, usimchukue huyo ndege pamoja na makinda yake.

  8. Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu.

  9. “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hayawezi kulinganishwa na mabawa na manyoya ya korongo.

  10. Huyataga mayai yake juu ya ardhi, na kuyaacha yapate joto mchangani,

  11. bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

  12. Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

  13. kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

  14. Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

  15. “Je, mwewe huruka kwa hekima yako na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini?

  16. Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu?

  17. Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku; majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake.

  18. Kutoka huko hutafuta chakula chake; macho yake hukiona kutoka mbali.

  19. Makinda yake hujilisha damu, na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.”

  20. Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima.

  21. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

  22. Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni,

  23. ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.

  24. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.

  25. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema