Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Birds

71 mistari · 107 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo.

  2. Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, miali ya moto watumishi wake.

  3. Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.

  4. Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.

  5. Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

  6. yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.

  7. Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.

  8. Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima.

  9. Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao.

  10. Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi.

  11. Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.

  12. Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

  13. tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

  14. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

  15. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  16. Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,

  17. kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.

  18. Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona!

  19. Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua.

  20. Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa.

  21. Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.