Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Birds: God provides for

12 mistari · 107 vipengele

Mistari kuhusu God provides for

  1. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.

  2. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema

  3. na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo.

  4. Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, miali ya moto watumishi wake.

  5. Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.

  6. Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.

  7. Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

  8. yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.

  9. Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.

  10. Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima.

  11. Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao.

  12. Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi.