Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 10:17takriban 1490 KK

    Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

  2. Hesabu 10:18takriban 1490 KK

    Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao.

  3. Hesabu 10:19takriban 1490 KK

    Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni,

  4. Hesabu 10:20takriban 1490 KK

    naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi.

  5. Hesabu 10:21takriban 1490 KK

    Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

  6. Hesabu 10:22takriban 1490 KK

    Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao.

  7. Hesabu 10:23takriban 1490 KK

    Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,

  8. Hesabu 10:24takriban 1490 KK

    naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.

  9. Hesabu 10:25takriban 1490 KK

    Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.

  10. Hesabu 10:26takriban 1490 KK

    Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,

  11. Hesabu 10:27takriban 1490 KK

    naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

  12. Hesabu 10:28takriban 1490 KK

    Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.

  13. Hesabu 10:29takriban 1490 KK

    Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo Bwana amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana Bwana ameahidi mambo mema kwa Israeli.”

  14. Hesabu 10:30takriban 1490 KK

    Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.”

  15. Hesabu 10:31takriban 1490 KK

    Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu.

  16. Hesabu 10:32takriban 1490 KK

    Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na Bwana.”

  17. Hesabu 10:33takriban 1490 KK

    Hivyo waliondoka kutoka mlima wa Bwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano la Bwana liliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.

  18. Hesabu 10:34takriban 1490 KK

    Wingu la Bwana lilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini.

  19. Hesabu 10:35takriban 1490 KK

    Wakati wowote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema, “Ee Bwana, inuka! Watesi wako na watawanyike; adui zako na wakimbie mbele zako.”

  20. Hesabu 10:36takriban 1490 KK

    Wakati wowote Sanduku liliposimama, alisema, “Ee Bwana, rudi, kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.”

  21. Hesabu 11:1takriban 1490 KK

    Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.

  22. Hesabu 11:2takriban 1490 KK

    Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika.

  23. Hesabu 11:3takriban 1490 KK

    Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao.

  24. Hesabu 11:4takriban 1490 KK

    Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule!

  25. Hesabu 11:5takriban 1490 KK

    Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu.