Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Samweli 23:20takriban 1055 KK

    Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

  2. 2 Samweli 23:21takriban 1055 KK

    Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.

  3. 2 Samweli 23:22takriban 1055 KK

    Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.

  4. 2 Samweli 23:23takriban 1055 KK

    Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

  5. 2 Samweli 23:24takriban 1055 KK

    Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo: Asaheli ndugu wa Yoabu; Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;

  6. 2 Samweli 23:25takriban 1055 KK

    Shama, Mharodi; Elika, Mharodi;

  7. 2 Samweli 23:26takriban 1055 KK

    Helesi, Mpalti; Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;

  8. 2 Samweli 23:27takriban 1055 KK

    Abiezeri kutoka Anathothi; Mebunai, Mhushathi;

  9. 2 Samweli 23:28takriban 1055 KK

    Salmoni, Mwahohi; Maharai, Mnetofathi;

  10. 2 Samweli 23:29takriban 1055 KK

    Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi; Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini;

  11. 2 Samweli 23:30takriban 1055 KK

    Benaya Mpirathoni; Hidai kutoka mabonde ya Gaashi;

  12. 2 Samweli 23:31takriban 1055 KK

    Abi-Alboni, Mwaribathi; Azmawethi, Mbarhumi;

  13. 2 Samweli 23:32takriban 1055 KK

    Eliaba, Mshaalboni; wana wa Yasheni; Yonathani

  14. 2 Samweli 23:33takriban 1055 KK

    mwana wa Shama, Mharari; Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;

  15. 2 Samweli 23:34takriban 1055 KK

    Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi; Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

  16. 2 Samweli 23:35takriban 1055 KK

    Hezro, Mkarmeli; Paarai, Mwarbi;

  17. 2 Samweli 23:36takriban 1055 KK

    Igali mwana wa Nathani kutoka Soba; Bani, Mgadi;

  18. 2 Samweli 23:37takriban 1055 KK

    Seleki, Mwamoni; Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mbeba silaha za Yoabu mwana wa Seruya;

  19. 2 Samweli 23:38takriban 1055 KK

    Ira, Mwithiri; Garebu, Mwithiri;

  20. 2 Samweli 23:39takriban 1055 KK

    na Uria, Mhiti. Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.

  21. 2 Samweli 24:1takriban 1017 KK

    Hasira ya Bwana ikawaka tena dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi dhidi yao, akisema, “Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.”

  22. 2 Samweli 24:2takriban 1017 KK

    Kwa hiyo mfalme akamwambia Yoabu, pamoja na majemadari wa jeshi aliokuwa nao, “Nendeni kwa makabila yote ya Israeli kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na mwandikishe watu wapiganaji, ili niweze kujua idadi yao.”

  23. 2 Samweli 24:3takriban 1017 KK

    Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “Bwana Mungu wako na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”

  24. 2 Samweli 24:4takriban 1017 KK

    Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu pamoja na majemadari wa jeshi, kwa hiyo wakaondoka mbele ya mfalme kuandikisha wapiganaji wa Israeli.

  25. 2 Samweli 24:5takriban 1017 KK

    Baada ya kuvuka Yordani, walipiga kambi karibu na Aroeri, kusini ya mji ulioko kwenye bonde jembamba, ndipo wakipitia Gadi, wakaenda hadi Yazeri.