Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Samweli 22:21takriban 1018 KK

    “Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.

  2. 2 Samweli 22:22takriban 1018 KK

    Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

  3. 2 Samweli 22:23takriban 1018 KK

    Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.

  4. 2 Samweli 22:24takriban 1018 KK

    Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.

  5. 2 Samweli 22:25takriban 1018 KK

    Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake.

  6. 2 Samweli 22:26takriban 1018 KK

    “Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,

  7. 2 Samweli 22:27takriban 1018 KK

    kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.

  8. 2 Samweli 22:28takriban 1018 KK

    Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe.

  9. 2 Samweli 22:29takriban 1018 KK

    Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga.

  10. 2 Samweli 22:30takriban 1018 KK

    Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.

  11. 2 Samweli 22:31takriban 1018 KK

    “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.

  12. 2 Samweli 22:32takriban 1018 KK

    Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?

  13. 2 Samweli 22:33takriban 1018 KK

    Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

  14. 2 Samweli 22:34takriban 1018 KK

    Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

  15. 2 Samweli 22:35takriban 1018 KK

    Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.

  16. 2 Samweli 22:36takriban 1018 KK

    Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua.

  17. 2 Samweli 22:37takriban 1018 KK

    Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.

  18. 2 Samweli 22:38takriban 1018 KK

    “Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

  19. 2 Samweli 22:39takriban 1018 KK

    Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu.

  20. 2 Samweli 22:40takriban 1018 KK

    Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.

  21. 2 Samweli 22:41takriban 1018 KK

    Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu.

  22. 2 Samweli 22:42takriban 1018 KK

    Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.

  23. 2 Samweli 22:43takriban 1018 KK

    Niliwaponda kama mavumbi ya nchi; niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani.

  24. 2 Samweli 22:44takriban 1018 KK

    “Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. Watu ambao sikuwajua wananitumikia,

  25. 2 Samweli 22:45takriban 1018 KK

    nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii.