- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1010–970 BC
The Reign of David
David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.
Mistari ya kipindi hiki
- 2 Samweli 21:18takriban 1018 KK
Baada ya muda, kukawa na vita nyingine na Wafilisti, huko Gobu. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Safu, mmoja wa wazao wa Warefai.
- 2 Samweli 21:19takriban 1018 KK
Katika vita vingine na Wafilisti huko Gobu, Elhanani mwana wa Yaare-Oregimu, Mbethlehemu, alimuua nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.
- 2 Samweli 21:20takriban 1018 KK
Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita kila mguu, jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.
- 2 Samweli 21:21takriban 1018 KK
Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.
- 2 Samweli 21:22takriban 1018 KK
Hawa wanne walikuwa wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.
- 2 Samweli 22:1takriban 1018 KK
Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli.
- 2 Samweli 22:2takriban 1018 KK
Akasema: “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu,
- 2 Samweli 22:3takriban 1018 KK
Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.
- 2 Samweli 22:4takriban 1018 KK
Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
- 2 Samweli 22:5takriban 1018 KK
“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
- 2 Samweli 22:6takriban 1018 KK
Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili.
- 2 Samweli 22:7takriban 1018 KK
Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.
- 2 Samweli 22:8takriban 1018 KK
“Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
- 2 Samweli 22:9takriban 1018 KK
Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.
- 2 Samweli 22:10takriban 1018 KK
Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
- 2 Samweli 22:11takriban 1018 KK
Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.
- 2 Samweli 22:12takriban 1018 KK
Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani.
- 2 Samweli 22:13takriban 1018 KK
Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.
- 2 Samweli 22:14takriban 1018 KK
Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
- 2 Samweli 22:15takriban 1018 KK
Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza.
- 2 Samweli 22:16takriban 1018 KK
Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
- 2 Samweli 22:17takriban 1018 KK
“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
- 2 Samweli 22:18takriban 1018 KK
Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
- 2 Samweli 22:19takriban 1018 KK
Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
- 2 Samweli 22:20takriban 1018 KK
Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.