Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 10:28takriban 33 BK

    Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.

  2. Mathayo 10:29takriban 33 BK

    Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua.

  3. Mathayo 10:30takriban 33 BK

    Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa.

  4. Mathayo 10:31takriban 33 BK

    Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

  5. Mathayo 10:32takriban 33 BK

    “Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

  6. Mathayo 10:33takriban 33 BK

    Lakini yeyote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

  7. Mathayo 10:34takriban 33 BK

    “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.

  8. Mathayo 10:35takriban 33 BK

    Kwa maana nimekuja kumfitini “ ‘mtu na babaye, binti na mamaye, mkwe na mama mkwe wake;

  9. Mathayo 10:36takriban 33 BK

    nao adui za mtu watakuwa ni wale watu wa nyumbani kwake.’

  10. Mathayo 10:37takriban 33 BK

    “Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu.

  11. Mathayo 10:38takriban 33 BK

    Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu.

  12. Mathayo 10:39takriban 33 BK

    Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.

  13. Mathayo 10:40takriban 33 BK

    “Mtu yeyote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi, na yeyote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma.

  14. Mathayo 10:41takriban 33 BK

    Mtu yeyote anayempokea nabii kwa kuwa ni nabii atapokea thawabu ya nabii, naye mtu anayempokea mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki atapokea thawabu ya mwenye haki.

  15. Mathayo 10:42takriban 33 BK

    Kama yeyote akimpa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, nawaambia, hataikosa thawabu yake.”

  16. Mathayo 11:1takriban 31 BK

    Baada ya Yesu kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

  17. Mathayo 11:2takriban 31 BK

    Yohana aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Kristo alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake

  18. Mathayo 11:3takriban 31 BK

    ili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

  19. Mathayo 11:4takriban 31 BK

    Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mnayosikia na kuyaona:

  20. Mathayo 11:5takriban 31 BK

    Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.

  21. Mathayo 11:6takriban 31 BK

    Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

  22. Mathayo 11:7takriban 31 BK

    Wale wanafunzi wa Yohana walipokuwa wanaondoka, Yesu akaanza kusema na makutano kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo?

  23. Mathayo 11:8takriban 31 BK

    Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme.

  24. Mathayo 11:9takriban 31 BK

    Basi mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii.

  25. Mathayo 11:10takriban 31 BK

    Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa: “ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako.’