Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 12:6takriban 31 BK

    Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa.

  2. Mathayo 12:7takriban 31 BK

    Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia,

  3. Mathayo 12:8takriban 31 BK

    kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

  4. Mathayo 12:9takriban 31 BK

    Yesu akaondoka mahali hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao,

  5. Mathayo 12:10takriban 31 BK

    na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, wakamuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?”

  6. Mathayo 12:11takriban 31 BK

    Yesu akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa?

  7. Mathayo 12:12takriban 31 BK

    Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”

  8. Mathayo 12:13takriban 31 BK

    Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine.

  9. Mathayo 12:14takriban 31 BK

    Lakini Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri baya juu ya Yesu jinsi watakavyoweza kumuua.

  10. Mathayo 12:15takriban 31 BK

    Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote,

  11. Mathayo 12:16takriban 31 BK

    akiwakataza wasiseme yeye ni nani.

  12. Mathayo 12:17takriban 31 BK

    Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

  13. Mathayo 12:18takriban 31 BK

    “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa.

  14. Mathayo 12:19takriban 31 BK

    Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

  15. Mathayo 12:20takriban 31 BK

    Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.

  16. Mathayo 12:21takriban 31 BK

    Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.”

  17. Mathayo 12:22takriban 31 BK

    Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona.

  18. Mathayo 12:23takriban 31 BK

    Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?”

  19. Mathayo 12:24takriban 31 BK

    Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo wachafu.”

  20. Mathayo 12:25takriban 31 BK

    Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama.

  21. Mathayo 12:26takriban 31 BK

    Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama?

  22. Mathayo 12:27takriban 31 BK

    Nami kama natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu.

  23. Mathayo 12:28takriban 31 BK

    Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.

  24. Mathayo 12:29takriban 31 BK

    “Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.

  25. Mathayo 12:30takriban 31 BK

    “Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya.