Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 10:3takriban 33 BK

    Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;

  2. Mathayo 10:4takriban 33 BK

    Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

  3. Mathayo 10:5takriban 33 BK

    Hawa kumi na wawili, Yesu aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.

  4. Mathayo 10:6takriban 33 BK

    Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea.

  5. Mathayo 10:7takriban 33 BK

    Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’

  6. Mathayo 10:8takriban 33 BK

    Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.

  7. Mathayo 10:9takriban 33 BK

    Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu.

  8. Mathayo 10:10takriban 33 BK

    Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.

  9. Mathayo 10:11takriban 33 BK

    “Mji wowote au kijiji chochote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake mpaka mtakapoondoka.

  10. Mathayo 10:12takriban 33 BK

    Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani.

  11. Mathayo 10:13takriban 33 BK

    Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.

  12. Mathayo 10:14takriban 33 BK

    Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo.

  13. Mathayo 10:15takriban 33 BK

    Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

  14. Mathayo 10:16takriban 33 BK

    “Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

  15. Mathayo 10:17takriban 33 BK

    “Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao.

  16. Mathayo 10:18takriban 33 BK

    Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa.

  17. Mathayo 10:19takriban 33 BK

    Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikiria mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo.

  18. Mathayo 10:20takriban 33 BK

    Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.

  19. Mathayo 10:21takriban 33 BK

    “Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe.

  20. Mathayo 10:22takriban 33 BK

    Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.

  21. Mathayo 10:23takriban 33 BK

    Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

  22. Mathayo 10:24takriban 33 BK

    “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, wala mtumishi hamzidi bwana wake.

  23. Mathayo 10:25takriban 33 BK

    Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli,je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake!

  24. Mathayo 10:26takriban 33 BK

    “Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana.

  25. Mathayo 10:27takriban 33 BK

    Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinongʼonwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba.