Rukia maudhui

circa 930–586 BC

The Divided Kingdom

The kingdom splits into Israel and Judah; prophets warn of judgment as both nations slowly drift into idolatry and exile.

1,722 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Nyakati 11:6takriban 975 KK

    Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa,

  2. 2 Nyakati 11:7takriban 975 KK

    Beth-Suri, Soko, Adulamu,

  3. 2 Nyakati 11:8takriban 975 KK

    Gathi, Maresha, Zifu,

  4. 2 Nyakati 11:9takriban 975 KK

    Adoraimu, Lakishi, Azeka,

  5. 2 Nyakati 11:10takriban 975 KK

    Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ndiyo iliyokuwa miji iliyojengewa ngome katika Yuda na Benyamini.

  6. 2 Nyakati 11:11takriban 975 KK

    Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na ghala za mahitaji ya vyakula, mafuta ya zeituni na divai.

  7. 2 Nyakati 11:12takriban 975 KK

    Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.

  8. 2 Nyakati 11:13takriban 974 KK

    Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake.

  9. 2 Nyakati 11:14takriban 974 KK

    Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Bwana.

  10. 2 Nyakati 11:15takriban 974 KK

    Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza.

  11. 2 Nyakati 11:16takriban 974 KK

    Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Bwana dhabihu, Mungu wa baba zao.

  12. 2 Nyakati 11:17takriban 975 KK

    Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu.

  13. 2 Nyakati 11:18takriban 975 KK

    Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese.

  14. 2 Nyakati 11:19takriban 975 KK

    Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu.

  15. 2 Nyakati 11:20takriban 975 KK

    Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi.

  16. 2 Nyakati 11:21takriban 975 KK

    Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini.

  17. 2 Nyakati 11:22takriban 975 KK

    Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme.

  18. 2 Nyakati 11:23takriban 975 KK

    Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi.

  19. 2 Nyakati 12:1takriban 972 KK

    Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria ya Bwana Mungu.

  20. 2 Nyakati 12:2takriban 970 KK

    Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Bwana, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu.

  21. 2 Nyakati 12:3takriban 970 KK

    Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi yaliyokuja pamoja naye kutoka Misri.

  22. 2 Nyakati 12:4takriban 970 KK

    Akateka miji ya Yuda yenye ngome akaendelea mpaka Yerusalemu.

  23. 2 Nyakati 12:5takriban 970 KK

    Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.’ ”

  24. 2 Nyakati 12:6takriban 970 KK

    Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Bwana Mungu ni mwenye haki.”

  25. 2 Nyakati 12:7takriban 970 KK

    Bwana Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Bwana likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kwa kupitia Shishaki.