Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Wagalatia 5:19takriban 58 BK

    Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi,

  2. Wagalatia 5:20takriban 58 BK

    kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

  3. Wagalatia 5:21takriban 58 BK

    husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

  4. Wagalatia 5:22takriban 58 BK

    Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

  5. Wagalatia 5:23takriban 58 BK

    upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

  6. Wagalatia 5:24takriban 58 BK

    Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake.

  7. Wagalatia 5:25takriban 58 BK

    Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.

  8. Wagalatia 5:26takriban 58 BK

    Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.

  9. Wagalatia 6:1takriban 58 BK

    Ndugu zangu, ikiwa mtu ameghafilika akatenda dhambi, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejesheni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa.

  10. Wagalatia 6:2takriban 58 BK

    Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Kristo.

  11. Wagalatia 6:3takriban 58 BK

    Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.

  12. Wagalatia 6:4takriban 58 BK

    Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine.

  13. Wagalatia 6:5takriban 58 BK

    Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.

  14. Wagalatia 6:6takriban 58 BK

    Basi, yeye afundishwaye katika neno na amshirikishe mwalimu wake mema yote.

  15. Wagalatia 6:7takriban 58 BK

    Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.

  16. Wagalatia 6:8takriban 58 BK

    Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

  17. Wagalatia 6:9takriban 58 BK

    Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

  18. Wagalatia 6:10takriban 58 BK

    Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

  19. Wagalatia 6:11takriban 58 BK

    Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!

  20. Wagalatia 6:12takriban 58 BK

    Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo.

  21. Wagalatia 6:13takriban 58 BK

    Hata wale waliotahiriwa wenyewe hawaitii sheria, lakini wanataka ninyi mtahiriwe ili wapate kujivuna kwa habari ya miili yenu.

  22. Wagalatia 6:14takriban 58 BK

    Mungu apishie mbali nisije nikajivunia kitu chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.

  23. Wagalatia 6:15takriban 58 BK

    Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu!

  24. Wagalatia 6:16takriban 58 BK

    Amani na rehema viwe na wote wanaofuata kanuni hii, na juu ya Israeli wa Mungu.

  25. Wagalatia 6:17takriban 58 BK

    Hatimaye, tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, kwa maana nachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu.