Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Wagalatia 4:25takriban 58 BK

    Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake.

  2. Wagalatia 4:26takriban 58 BK

    Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu.

  3. Wagalatia 4:27takriban 58 BK

    Kwa maana imeandikwa: “Furahi, ewe mwanamke tasa, wewe usiyezaa; paza sauti, na kuimba kwa furaha, wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa; kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume.”

  4. Wagalatia 4:28takriban 58 BK

    Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi.

  5. Wagalatia 4:29takriban 58 BK

    Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa.

  6. Wagalatia 4:30takriban 58 BK

    Lakini Maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.”

  7. Wagalatia 4:31takriban 58 BK

    Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali wa yule aliye huru.

  8. Wagalatia 5:1takriban 58 BK

    Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.

  9. Wagalatia 5:2takriban 58 BK

    Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote.

  10. Wagalatia 5:3takriban 58 BK

    Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote.

  11. Wagalatia 5:4takriban 58 BK

    Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.

  12. Wagalatia 5:5takriban 58 BK

    Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki.

  13. Wagalatia 5:6takriban 58 BK

    Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

  14. Wagalatia 5:7takriban 58 BK

    Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli?

  15. Wagalatia 5:8takriban 58 BK

    Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita.

  16. Wagalatia 5:9takriban 58 BK

    “Chachu kidogo huchachua donge zima.”

  17. Wagalatia 5:10takriban 58 BK

    Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.

  18. Wagalatia 5:11takriban 58 BK

    Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa.

  19. Wagalatia 5:12takriban 58 BK

    Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!

  20. Wagalatia 5:13takriban 58 BK

    Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.

  21. Wagalatia 5:14takriban 58 BK

    Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

  22. Wagalatia 5:15takriban 58 BK

    Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.

  23. Wagalatia 5:16takriban 58 BK

    Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

  24. Wagalatia 5:17takriban 58 BK

    Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.

  25. Wagalatia 5:18takriban 58 BK

    Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.