Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 30:13takriban 1747 KK

    Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.

  2. Mwanzo 30:14takriban 1748 KK

    Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”

  3. Mwanzo 30:15takriban 1748 KK

    Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kumtwaa mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?” Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.”

  4. Mwanzo 30:16takriban 1748 KK

    Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule.

  5. Mwanzo 30:17takriban 1747 KK

    Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano.

  6. Mwanzo 30:18takriban 1747 KK

    Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.

  7. Mwanzo 30:19takriban 1747 KK

    Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita.

  8. Mwanzo 30:20takriban 1746 KK

    Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.

  9. Mwanzo 30:21takriban 1745 KK

    Baadaye akamzaa mtoto wa kike akamwita Dina.

  10. Mwanzo 30:22takriban 1745 KK

    Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.

  11. Mwanzo 30:23takriban 1745 KK

    Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

  12. Mwanzo 30:24takriban 1745 KK

    Akamwita Yosefu na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.”

  13. Mwanzo 30:25takriban 1745 KK

    Baada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu.

  14. Mwanzo 30:26takriban 1745 KK

    Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.”

  15. Mwanzo 30:27takriban 1745 KK

    Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba Bwana amenibariki kwa sababu yako.”

  16. Mwanzo 30:28takriban 1745 KK

    Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.”

  17. Mwanzo 30:29takriban 1745 KK

    Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi ambavyo nimekutumikia na jinsi ambavyo wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu.

  18. Mwanzo 30:30takriban 1745 KK

    Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, naye Bwana amekubariki popote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?”

  19. Mwanzo 30:31takriban 1745 KK

    Labani akamuuliza, “Nikupe nini?” Yakobo akamjibu, “Usinipe chochote lakini kama utanifanyia jambo hili moja, nitaendelea kuchunga na kuyaangalia makundi yako.

  20. Mwanzo 30:32takriban 1745 KK

    Niruhusu nipite katika makundi yako yote leo niondoe humo kila kondoo mwenye mabakabaka au madoadoa, kila mwana-kondoo mweusi na kila mbuzi mwenye madoadoa au mabakabaka. Hawa watakuwa ujira wangu.

  21. Mwanzo 30:33takriban 1745 KK

    Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi yeyote wangu ambaye hana mabakabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.”

  22. Mwanzo 30:34takriban 1745 KK

    Labani akasema, “Ninakubali na iwe kama ulivyosema.”

  23. Mwanzo 30:35takriban 1745 KK

    Siku ile ile Yakobo akawaondoa beberu wote waliokuwa na mistari au madoadoa na mbuzi wake wote waliokuwa na mistari au madoadoa (wote waliokuwa na alama nyeupe juu yao) na wana-kondoo weusi wote, akawaweka chini ya uangalizi wa wanawe.

  24. Mwanzo 30:36takriban 1745 KK

    Kisha Labani akamwacha Yakobo kwa mwendo wa safari ya siku tatu kati yake na Yakobo, wakati Yakobo akiendelea kuchunga lile kundi la Labani lililobaki.

  25. Mwanzo 30:37takriban 1745 KK

    Hata hivyo, Yakobo, akachukua fito mbichi zilizokatwa wakati huo huo za miti ya mlubna, mlozi na mwaramoni akazibambua ili mistari myeupe ionekane katika fito hizo.