Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 29:23takriban 1753 KK

    Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili.

  2. Mwanzo 29:24takriban 1753 KK

    Naye Labani akamtoa Zilpa, mtumishi wake wa kike, kuwa mtumishi wa Lea, binti yake.

  3. Mwanzo 29:25takriban 1753 KK

    Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?”

  4. Mwanzo 29:26takriban 1753 KK

    Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa.

  5. Mwanzo 29:27takriban 1753 KK

    Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.”

  6. Mwanzo 29:28takriban 1753 KK

    Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.

  7. Mwanzo 29:29takriban 1753 KK

    Labani akamtoa Bilha mtumishi wake wa kike kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake.

  8. Mwanzo 29:30takriban 1753 KK

    Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli zaidi kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba.

  9. Mwanzo 29:31takriban 1753 KK

    Bwana alipoona kwamba Lea hapendwi, akampa watoto, lakini Raheli alikuwa tasa.

  10. Mwanzo 29:32takriban 1752 KK

    Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni, kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Bwana ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”

  11. Mwanzo 29:33takriban 1751 KK

    Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu Bwana alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.

  12. Mwanzo 29:34takriban 1750 KK

    Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.

  13. Mwanzo 29:35takriban 1749 KK

    Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu Bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.

  14. Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!”

  15. Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?”

  16. Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”

  17. Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili,

  18. Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana.

  19. Mwanzo 30:6takriban 1748 KK

    Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.

  20. Mwanzo 30:7takriban 1747 KK

    Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

  21. Mwanzo 30:8takriban 1747 KK

    Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.

  22. Mwanzo 30:9takriban 1748 KK

    Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake.

  23. Mwanzo 30:10takriban 1748 KK

    Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana.

  24. Mwanzo 30:11takriban 1748 KK

    Ndipo Lea akasema, “Hii ni bahati nzuri aje!” Kwa hiyo akamwita Gadi.

  25. Mwanzo 30:12takriban 1748 KK

    Mtumishi wa kike wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili.