- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1900–1700 BC
Jacob, Joseph & Egypt
Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.
Mistari ya kipindi hiki
- Mwanzo 46:7takriban 1706 KK
Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri.
- Mwanzo 46:8takriban 1706 KK
Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.
- Mwanzo 46:9takriban 1706 KK
Wana wa Reubeni ni: Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.
- Mwanzo 46:10takriban 1706 KK
Wana wa Simeoni ni: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani.
- Mwanzo 46:11takriban 1706 KK
Wana wa Lawi ni: Gershoni, Kohathi na Merari.
- Mwanzo 46:12takriban 1706 KK
Wana wa Yuda ni: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi ni: Hesroni na Hamuli.
- Mwanzo 46:13takriban 1706 KK
Wana wa Isakari ni: Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.
- Mwanzo 46:14takriban 1706 KK
Wana wa Zabuloni ni: Seredi, Eloni na Yaleeli.
- Mwanzo 46:15takriban 1706 KK
Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.
- Mwanzo 46:16takriban 1706 KK
Wana wa Gadi ni: Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.
- Mwanzo 46:17takriban 1706 KK
Wana wa Asheri ni: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. Wana wa Beria ni: Heberi na Malkieli.
- Mwanzo 46:18takriban 1706 KK
Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita.
- Mwanzo 46:19takriban 1706 KK
Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni: Yosefu na Benyamini.
- Mwanzo 46:20takriban 1706 KK
Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu.
- Mwanzo 46:21takriban 1706 KK
Wana wa Benyamini ni: Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi.
- Mwanzo 46:22takriban 1706 KK
Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne.
- Mwanzo 46:23takriban 1706 KK
Mwana wa Dani ni: Hushimu.
- Mwanzo 46:24takriban 1706 KK
Wana wa Naftali ni: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu.
- Mwanzo 46:25takriban 1706 KK
Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba.
- Mwanzo 46:26takriban 1706 KK
Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita.
- Mwanzo 46:27takriban 1706 KK
Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini.
- Mwanzo 46:28takriban 1706 KK
Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni,
- Mwanzo 46:29takriban 1706 KK
gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.
- Mwanzo 46:30takriban 1706 KK
Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.”
- Mwanzo 46:31takriban 1706 KK
Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu.