Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Wife

171 mistari · 13 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

  2. Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.

  3. Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.

  4. Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

  5. Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

  6. Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.

  7. Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

  8. Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

  9. Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.

  10. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

  11. Huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu.

  12. Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, mumewe pia humsifu, akisema:

  13. “Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini wewe umewapita wote.”

  14. Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

  15. Mpe thawabu anayostahili, nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.

  16. Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

  17. Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe.

  18. Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.

  19. Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.

  20. Nasema haya kama ushauri na si amri.

  21. Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe.

  22. Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.

  23. Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache.

  24. Naye mwanamke aaminiye kama ameolewa na mwanaume asiyeamini na huyo mume anakubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimwache.

  25. Kwa maana huyo mume asiyeamini anatakaswa kupitia mkewe, naye mke asiyeamini anatakaswa kupitia mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wenu wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu.