Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Wife

171 mistari · 13 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.

  2. “Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitabadilika, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahasuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kumliko yeye.

  3. Kisha mbiu hii ya mfalme itakapotangazwa katika himaya yake iliyo kubwa sana, wanawake wote watawaheshimu waume zao, kuanzia mdogo hadi mkubwa.”

  4. Mfalme na wakuu wake walipendezwa na shauri hili, hivyo basi mfalme akafanya kama Memukani alivyopendekeza.

  5. Alipeleka barua katika sehemu zote za ufalme wake, kwa kila jimbo kwa maandishi yake mwenyewe na kwa kila watu katika lugha yao wenyewe, akitangaza kwa msemo wa kila watu kwamba inampasa kila mwanaume kuwa mtawala wa nyumba yake mwenyewe.

  6. Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.

  7. Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.

  8. Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

  9. Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

  10. Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.

  11. Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

  12. Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

  13. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

  14. Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.

  15. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

  16. “Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:

  17. Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula,

  18. mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.

  19. Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.

  20. Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu chochote cha thamani.

  21. Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake.

  22. Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.

  23. Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.

  24. Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

  25. Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.