Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflicted Saints

122 mistari · 31 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

  2. Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

  3. Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema yake na kuniweka juu kwenye mwamba.

  4. Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Bwana na kumsifu.

  5. Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.

  6. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  7. Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,

  8. huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.

  9. Nilinyamaza kimya, sikufumbua kinywa changu, kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.

  10. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

  11. Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

  12. na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”

  13. Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako?

  14. Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

  15. Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?

  16. Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu.

  17. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu,

  18. Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe.

  19. Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

  20. Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu:

  21. nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi na nilizotamka kwa kinywa changu nilipokuwa katika shida.

  22. Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono na sadaka za kondoo dume, nitakutolea mafahali na mbuzi.

  23. Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena.

  24. Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena.

  25. Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze.