Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Afflicted Saints: God comforts

6 mistari · 31 vipengele

Mistari kuhusu God comforts

  1. Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu; furahi, ee dunia; pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima! Kwa maana Bwana anawafariji watu wake, naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.

  2. Kisha wanawali watacheza na kufurahi, vijana waume na wazee pia. Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni.

  3. Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

  4. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.

  5. Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo.

  6. Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito.