Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Timotheo 1:10takriban 65 BK

    kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,

  2. 1 Timotheo 1:11takriban 65 BK

    ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi nimewekewa amana.

  3. 1 Timotheo 1:12takriban 65 BK

    Namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona mwaminifu, akaniteua kwa kazi yake.

  4. 1 Timotheo 1:13takriban 65 BK

    Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu.

  5. 1 Timotheo 1:14takriban 65 BK

    Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.

  6. 1 Timotheo 1:15takriban 65 BK

    Msemo huu ni wa kweli na unaostahili kukubalika, usemao kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote.

  7. 1 Timotheo 1:16takriban 65 BK

    Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele.

  8. 1 Timotheo 1:17takriban 65 BK

    Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.

  9. 1 Timotheo 1:18takriban 65 BK

    Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri,

  10. 1 Timotheo 1:19takriban 65 BK

    ukiishikilia imani na dhamiri njema, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao.

  11. 1 Timotheo 1:20takriban 65 BK

    Miongoni mwao wako Himenayo na Aleksanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.

  12. 1 Timotheo 2:1takriban 65 BK

    Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote:

  13. 1 Timotheo 2:2takriban 65 BK

    kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.

  14. 1 Timotheo 2:3takriban 65 BK

    Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu,

  15. 1 Timotheo 2:4takriban 65 BK

    anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli.

  16. 1 Timotheo 2:5takriban 65 BK

    Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu,

  17. 1 Timotheo 2:6takriban 65 BK

    aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao.

  18. 1 Timotheo 2:7takriban 65 BK

    Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.

  19. 1 Timotheo 2:8takriban 65 BK

    Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.

  20. 1 Timotheo 2:9takriban 65 BK

    Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa,

  21. 1 Timotheo 2:10takriban 65 BK

    bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

  22. 1 Timotheo 2:11takriban 65 BK

    Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote.

  23. 1 Timotheo 2:12takriban 65 BK

    Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya.

  24. 1 Timotheo 2:13takriban 65 BK

    Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva.

  25. 1 Timotheo 2:14takriban 65 BK

    Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji.