Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Warumi 2:19takriban 60 BK

    kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani,

  2. Warumi 2:20takriban 60 BK

    mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una maarifa ya kweli katika hiyo sheria,

  3. Warumi 2:21takriban 60 BK

    basi wewe, uwafundishaye wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, wewe mwenyewe waiba?

  4. Warumi 2:22takriban 60 BK

    Wewe usemaye mtu asizini, wewe mwenyewe wazini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, wafanya jambo la kumchukiza katika mahekalu?

  5. Warumi 2:23takriban 60 BK

    Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria?

  6. Warumi 2:24takriban 60 BK

    Kama ilivyoandikwa, “Kwa ajili yenu ninyi, Jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa watu wa Mataifa.”

  7. Warumi 2:25takriban 60 BK

    Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

  8. Warumi 2:26takriban 60 BK

    Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo sheria inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa?

  9. Warumi 2:27takriban 60 BK

    Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.

  10. Warumi 2:28takriban 60 BK

    Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje, wala tohara ya kweli si kitu cha nje au cha kimwili.

  11. Warumi 2:29takriban 60 BK

    Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.

  12. Warumi 3:1takriban 60 BK

    Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara?

  13. Warumi 3:2takriban 60 BK

    Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu.

  14. Warumi 3:3takriban 60 BK

    Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu?

  15. Warumi 3:4takriban 60 BK

    La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena, na ukashinde utoapo hukumu.”

  16. Warumi 3:5takriban 60 BK

    Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.)

  17. Warumi 3:6takriban 60 BK

    La hasha! Kama hivyo ndivyo ilivyo, Mungu angehukumuje ulimwengu?

  18. Warumi 3:7takriban 60 BK

    Mtu aweza kuuliza, “Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha kweli ya Mungu na kuzidisha utukufu wake, kwa nini basi mimi nahukumiwa kuwa mwenye dhambi?”

  19. Warumi 3:8takriban 60 BK

    Nasi kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili mema yapate kuja?” Wao wanastahili hukumu yao.

  20. Warumi 3:9takriban 60 BK

    Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi.

  21. Warumi 3:10takriban 60 BK

    Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

  22. Warumi 3:11takriban 60 BK

    Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

  23. Warumi 3:12takriban 60 BK

    Wote wamepotoka, wote wameoza pamoja; hakuna atendaye mema, naam, hakuna hata mmoja.”

  24. Warumi 3:13takriban 60 BK

    “Makoo yao ni makaburi wazi; kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.” “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”

  25. Warumi 3:14takriban 60 BK

    “Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”