Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Young Men

347 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Jawabu la uaminifu ni kama busu la midomoni.

  2. Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako.

  3. Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya.

  4. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”

  5. Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,

  6. miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.

  7. Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:

  8. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

  9. hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

  10. Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau.

  11. Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

  12. Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.

  13. Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

  14. “Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, ee mwana wa nadhiri zangu,

  15. Usitumie nguvu zako kwa wanawake, uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

  16. Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’ Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

  17. Atazikwa maziko ya punda: ataburutwa na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.”

  18. “Panda Lebanoni ukapige kelele, sauti yako na isikike huko Bashani, piga kelele toka Abarimu, kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa.

  19. Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; hujanitii mimi.

  20. Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

  21. Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”

  22. Yule mtu akamuuliza, “Amri zipi?” Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,

  23. waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.”

  24. Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?”

  25. Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”