Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Young Men

347 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

  2. Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana aletaye aibu na fedheha.

  3. Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.

  4. Utukufu wa vijana ni nguvu zao, mvi ni fahari ya uzee.

  5. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi,

  6. utu wangu wa ndani utafurahi, wakati midomo yako itakapozungumza lililo sawa.

  7. Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.

  8. Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.

  9. Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.

  10. Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa,

  11. kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara.

  12. Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

  13. Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu.

  14. Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa, naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

  15. Baba yako na mama yako na wafurahi, mama aliyekuzaa na ashangilie!

  16. Mwanangu, nipe moyo wako, macho yako na yafuate njia zangu,

  17. kwa maana kahaba ni shimo refu na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba.

  18. Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia, naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.

  19. Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu?

  20. Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

  21. Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu!

  22. Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

  23. Macho yako yataona mambo mageni na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.

  24. Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, alalaye juu ya kamba ya merikebu.

  25. Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?”