Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Young Men

347 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.

  2. Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.

  3. (Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;

  4. mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)

  5. Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:

  6. “Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.

  7. Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!

  8. Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.

  9. Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.

  10. Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!

  11. Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.

  12. Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

  13. Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.

  14. Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,

  15. mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.

  16. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.

  17. Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.

  18. Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.

  19. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

  20. Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.

  21. Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye, bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

  22. Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.

  23. Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.

  24. Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.

  25. Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.