Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Prudence

192 mistari · 40 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa.

  2. Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.

  3. Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.

  4. Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.

  5. Kama ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia.

  6. Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako,

  7. na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi.

  8. Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

  9. Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.

  10. kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi.

  11. Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako.

  12. usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha?

  13. Kama ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine,

  14. ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka.

  15. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.

  16. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.

  17. Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.

  18. Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.

  19. Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.

  20. Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

  21. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

  22. Usiwe mwenye haki kupita kiasi, wala usiwe na hekima kupita kiasi: kwa nini kujiangamiza mwenyewe?

  23. Usiwe mwovu kupita kiasi, wala usiwe mpumbavu: kwa nini kufa kabla ya wakati wako?

  24. Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu.

  25. Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lolote apendalo.