Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 24:13takriban 33 BK

    lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.

  2. Mathayo 24:14takriban 33 BK

    Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.

  3. Mathayo 24:15takriban 33 BK

    “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),

  4. Mathayo 24:16takriban 33 BK

    basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani.

  5. Mathayo 24:17takriban 33 BK

    Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba.

  6. Mathayo 24:18takriban 33 BK

    Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake.

  7. Mathayo 24:19takriban 33 BK

    Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo!

  8. Mathayo 24:20takriban 33 BK

    Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato.

  9. Mathayo 24:21takriban 33 BK

    Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe.

  10. Mathayo 24:22takriban 33 BK

    Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa.

  11. Mathayo 24:23takriban 33 BK

    Wakati huo kama mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ Au, ‘Kristo yuko kule,’ msisadiki.

  12. Mathayo 24:24takriban 33 BK

    Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa.

  13. Mathayo 24:25takriban 33 BK

    Angalieni, nimekwisha kuwaambia mapema.

  14. Mathayo 24:26takriban 33 BK

    “Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki.

  15. Mathayo 24:27takriban 33 BK

    Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

  16. Mathayo 24:28takriban 33 BK

    Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai.

  17. Mathayo 24:29takriban 33 BK

    “Mara baada ya dhiki ya siku zile, “ ‘jua litatiwa giza, nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’

  18. Mathayo 24:30takriban 33 BK

    “Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu.

  19. Mathayo 24:31takriban 33 BK

    Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

  20. Mathayo 24:32takriban 33 BK

    “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.

  21. Mathayo 24:33takriban 33 BK

    Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni.

  22. Mathayo 24:34takriban 33 BK

    Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.

  23. Mathayo 24:35takriban 33 BK

    Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

  24. Mathayo 24:36takriban 33 BK

    “Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.

  25. Mathayo 24:37takriban 33 BK

    Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.