Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 23:2takriban 33 BK

    “Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Mose,

  2. Mathayo 23:3takriban 33 BK

    hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri.

  3. Mathayo 23:4takriban 33 BK

    Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza.

  4. Mathayo 23:5takriban 33 BK

    “Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.

  5. Mathayo 23:6takriban 33 BK

    Wanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi.

  6. Mathayo 23:7takriban 33 BK

    Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Rabi.’

  7. Mathayo 23:8takriban 33 BK

    “Lakini ninyi msiitwe ‘Rabi,’ kwa sababu mnaye Bwana mmoja na ninyi nyote ni ndugu.

  8. Mathayo 23:9takriban 33 BK

    Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba,’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.

  9. Mathayo 23:10takriban 33 BK

    Wala msiitwe ‘Mwalimu,’ kwa maana mnaye mwalimu mmoja tu, ndiye Kristo.

  10. Mathayo 23:11takriban 33 BK

    Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.

  11. Mathayo 23:12takriban 33 BK

    Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa.

  12. Mathayo 23:13takriban 33 BK

    “Lakini ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Kwa maana mnawafungia watu milango ya Ufalme wa Mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, nao wale wanaotaka kuingia mnawazuia. [

  13. Mathayo 23:14takriban 33 BK

    Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo hukumu yenu itakuwa kuu zaidi.]

  14. Mathayo 23:15takriban 33 BK

    “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa jehanamu mara mbili kuliko ninyi!

  15. Mathayo 23:16takriban 33 BK

    “Ole wenu, viongozi vipofu! Ninyi mwasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, amefungwa kwa kiapo chake.’

  16. Mathayo 23:17takriban 33 BK

    Ninyi vipofu wapumbavu! Ni kipi kilicho kikuu zaidi: ni ile dhahabu, au ni lile Hekalu linaloifanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?

  17. Mathayo 23:18takriban 33 BK

    Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu; lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu, amefungwa kwa kiapo chake’

  18. Mathayo 23:19takriban 33 BK

    Ninyi vipofu! Ni kipi kikuu zaidi: ni sadaka, au ni madhabahu yanayoifanya hiyo sadaka kuwa takatifu?

  19. Mathayo 23:20takriban 33 BK

    Kwa hiyo, mtu aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hayo madhabahu na vitu vyote vilivyo juu yake.

  20. Mathayo 23:21takriban 33 BK

    Naye mtu aapaye kwa Hekalu, huapa kwa hilo Hekalu na kwa huyo akaaye ndani yake.

  21. Mathayo 23:22takriban 33 BK

    Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.

  22. Mathayo 23:23takriban 33 BK

    “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo.

  23. Mathayo 23:24takriban 33 BK

    Ninyi viongozi vipofu, mnachuja kiroboto lakini mnameza ngamia!

  24. Mathayo 23:25takriban 33 BK

    “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na kutokuwa na kiasi.

  25. Mathayo 23:26takriban 33 BK

    Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia.