Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 23:27takriban 33 BK

    “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo yanapendeza kwa nje, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu.

  2. Mathayo 23:28takriban 33 BK

    Vivyo hivyo, kwa nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

  3. Mathayo 23:29takriban 33 BK

    “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.

  4. Mathayo 23:30takriban 33 BK

    Nanyi mwasema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu, tusingalikuwa tumeshiriki katika kumwaga damu ya manabii!’

  5. Mathayo 23:31takriban 33 BK

    Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii.

  6. Mathayo 23:32takriban 33 BK

    Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu!

  7. Mathayo 23:33takriban 33 BK

    “Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jehanamu?

  8. Mathayo 23:34takriban 33 BK

    Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.

  9. Mathayo 23:35takriban 33 BK

    Hivyo ile damu ya wenye haki wote iliyomwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zekaria mwana wa Barakia, mliyemuua kati ya patakatifu na madhabahu, itawajia juu yenu.

  10. Mathayo 23:36takriban 33 BK

    Amin, nawaambia, haya yote yatakuja juu ya kizazi hiki.

  11. Mathayo 23:37takriban 33 BK

    “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

  12. Mathayo 23:38takriban 33 BK

    Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa.

  13. Mathayo 23:39takriban 33 BK

    Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena tangu sasa mpaka mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana.’ ”

  14. Mathayo 24:1takriban 33 BK

    Yesu akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu.

  15. Mathayo 24:2takriban 33 BK

    Ndipo Yesu akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

  16. Mathayo 24:3takriban 33 BK

    Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

  17. Mathayo 24:4takriban 33 BK

    Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye.

  18. Mathayo 24:5takriban 33 BK

    Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’nao watawadanganya wengi.

  19. Mathayo 24:6takriban 33 BK

    Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado.

  20. Mathayo 24:7takriban 33 BK

    Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.

  21. Mathayo 24:8takriban 33 BK

    Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

  22. Mathayo 24:9takriban 33 BK

    “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.

  23. Mathayo 24:10takriban 33 BK

    Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana.

  24. Mathayo 24:11takriban 33 BK

    Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi.

  25. Mathayo 24:12takriban 33 BK

    Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa,