Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 24:38takriban 33 BK

    Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina.

  2. Mathayo 24:39takriban 33 BK

    Nao hawakujua lolote mpaka gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu.

  3. Mathayo 24:40takriban 33 BK

    Watu wawili watakuwa shambani, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.

  4. Mathayo 24:41takriban 33 BK

    Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.

  5. Mathayo 24:42takriban 33 BK

    “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu.

  6. Mathayo 24:43takriban 33 BK

    Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa.

  7. Mathayo 24:44takriban 33 BK

    Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.

  8. Mathayo 24:45takriban 33 BK

    “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?

  9. Mathayo 24:46takriban 33 BK

    Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.

  10. Mathayo 24:47takriban 33 BK

    Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote.

  11. Mathayo 24:48takriban 33 BK

    Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’

  12. Mathayo 24:49takriban 33 BK

    kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi.

  13. Mathayo 24:50takriban 33 BK

    Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua.

  14. Mathayo 24:51takriban 33 BK

    Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.

  15. Mathayo 25:1takriban 33 BK

    “Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi.

  16. Mathayo 25:2takriban 33 BK

    Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.

  17. Mathayo 25:3takriban 33 BK

    Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,

  18. Mathayo 25:4takriban 33 BK

    lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo.

  19. Mathayo 25:5takriban 33 BK

    Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

  20. Mathayo 25:6takriban 33 BK

    “Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’

  21. Mathayo 25:7takriban 33 BK

    “Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.

  22. Mathayo 25:8takriban 33 BK

    Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’

  23. Mathayo 25:9takriban 33 BK

    “Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’

  24. Mathayo 25:10takriban 33 BK

    “Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

  25. Mathayo 25:11takriban 33 BK

    “Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’