Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Isaya 2:20takriban 759 KK

    Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.

  2. Isaya 2:21takriban 759 KK

    Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.

  3. Isaya 2:22takriban 759 KK

    Acheni kumtumainia mwanadamu, ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake. Yeye ana thamani gani?

  4. Isaya 3:1takriban 759 KK

    Tazama sasa, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda upatikanaji wa mahitaji na misaada, upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,

  5. Isaya 3:2takriban 759 KK

    shujaa na mtu wa vita, mwamuzi na nabii, mwaguzi na mzee,

  6. Isaya 3:3takriban 759 KK

    jemadari wa kikosi cha watu hamsini na mtu mwenye cheo, mshauri, fundi stadi na mlozi mjanja.

  7. Isaya 3:4takriban 759 KK

    Nitawafanya wavulana wawe maafisa wao, watoto ndio watakaowatawala.

  8. Isaya 3:5takriban 759 KK

    Watu wataoneana wao kwa wao: mtu dhidi ya mtu, na jirani dhidi ya jirani yake. Kijana atainuka dhidi ya mzee, mtu mnyonge dhidi ya mtu mwenye heshima.

  9. Isaya 3:6takriban 759 KK

    Mtu atamkamata mmoja wa ndugu zake katika nyumba ya baba yake na kusema, “Unalo joho, sasa uwe kiongozi wetu, tawala lundo hili la magofu!”

  10. Isaya 3:7takriban 759 KK

    Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina uponyaji. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

  11. Isaya 3:8takriban 759 KK

    Yerusalemu inapepesuka, Yuda inaanguka; maneno yao na matendo yao ni kinyume na Bwana, wakiudharau uwepo wake uliotukuka.

  12. Isaya 3:9takriban 759 KK

    Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.

  13. Isaya 3:10takriban 759 KK

    Waambie wanyofu itakuwa heri kwao, kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao.

  14. Isaya 3:11takriban 759 KK

    Ole kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao! Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.

  15. Isaya 3:12takriban 759 KK

    Vijana wanawatesa watu wangu, wanawake wanawatawala. Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha, wanawapoteza njia.

  16. Isaya 3:13takriban 759 KK

    Bwana anachukua nafasi yake mahakamani, anasimama kuhukumu watu.

  17. Isaya 3:14takriban 759 KK

    Bwana anaingia katika hukumu dhidi ya wazee na viongozi wa watu wake: “Ninyi ndio mlioharibu shamba langu la mizabibu, mali zilizonyangʼanywa maskini zimo nyumbani mwenu.

  18. Isaya 3:15takriban 759 KK

    Mnamaanisha nini kuwaponda watu wangu na kuzisaga nyuso za maskini?” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  19. Isaya 3:16takriban 759 KK

    Bwana asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wanatembea kwa hatua za madaha, wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.

  20. Isaya 3:17takriban 759 KK

    Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni; Bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”

  21. Isaya 3:18takriban 759 KK

    Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo,

  22. Isaya 3:19takriban 759 KK

    vipuli, vikuku, shela,

  23. Isaya 3:20takriban 759 KK

    vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi,

  24. Isaya 3:21takriban 759 KK

    pete zenye muhuri, pete za puani,

  25. Isaya 3:22takriban 759 KK

    majoho mazuri, mitandio, mavazi, kifuko cha kutilia fedha,