Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Isaya 1:26takriban 759 KK

    Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani, nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni. Baadaye utaitwa, Mji wa Haki, Mji Mwaminifu.”

  2. Isaya 1:27takriban 759 KK

    Sayuni itakombolewa kwa haki, wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu.

  3. Isaya 1:28takriban 759 KK

    Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa, nao wanaomwacha Bwana wataangamia.

  4. Isaya 1:29takriban 759 KK

    “Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni ambayo mlifurahia, mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizozichagua.

  5. Isaya 1:30takriban 759 KK

    Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, kama bustani isiyokuwa na maji.

  6. Isaya 1:31takriban 759 KK

    Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto, na kazi yake kama cheche ya moto; vyote vitaungua pamoja, wala hakuna wa kuuzima huo moto.”

  7. Isaya 2:1takriban 759 KK

    Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:

  8. Isaya 2:2takriban 759 KK

    Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko.

  9. Isaya 2:3takriban 759 KK

    Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

  10. Isaya 2:4takriban 759 KK

    Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.

  11. Isaya 2:5takriban 759 KK

    Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.

  12. Isaya 2:6takriban 759 KK

    Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.

  13. Isaya 2:7takriban 759 KK

    Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao.

  14. Isaya 2:8takriban 759 KK

    Nchi yao imejaa sanamu, wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.

  15. Isaya 2:9takriban 759 KK

    Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.

  16. Isaya 2:10takriban 759 KK

    Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake!

  17. Isaya 2:11takriban 759 KK

    Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.

  18. Isaya 2:12takriban 759 KK

    Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),

  19. Isaya 2:13takriban 759 KK

    kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,

  20. Isaya 2:14takriban 759 KK

    kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,

  21. Isaya 2:15takriban 759 KK

    kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,

  22. Isaya 2:16takriban 759 KK

    kwa kila meli ya biashara, na kila chombo cha baharini cha fahari.

  23. Isaya 2:17takriban 759 KK

    Majivuno ya mwanadamu yatashushwa, na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,

  24. Isaya 2:18takriban 759 KK

    nazo sanamu zitatoweka kabisa.

  25. Isaya 2:19takriban 759 KK

    Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.