Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 39:34takriban 1491 KK

    kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, kifuniko cha ngozi za pomboo, pazia la kufunikia;

  2. Kutoka 39:35takriban 1491 KK

    Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema,

  3. Kutoka 39:36takriban 1491 KK

    meza pamoja na vyombo vyake vyote na mikate ya Wonyesho;

  4. Kutoka 39:37takriban 1491 KK

    kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa;

  5. Kutoka 39:38takriban 1491 KK

    madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri na pazia la ingilio la hema;

  6. Kutoka 39:39takriban 1491 KK

    madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, sinia, na tako lake;

  7. Kutoka 39:40takriban 1491 KK

    mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania;

  8. Kutoka 39:41takriban 1491 KK

    na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.

  9. Kutoka 39:42takriban 1491 KK

    Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose.

  10. Kutoka 39:43takriban 1491 KK

    Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki.

  11. Kutoka 40:1takriban 1491 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose:

  12. Kutoka 40:2takriban 1491 KK

    “Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.

  13. Kutoka 40:3takriban 1491 KK

    Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake.

  14. Kutoka 40:4takriban 1491 KK

    Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake.

  15. Kutoka 40:5takriban 1491 KK

    Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu.

  16. Kutoka 40:6takriban 1491 KK

    “Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania;

  17. Kutoka 40:7takriban 1491 KK

    weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake.

  18. Kutoka 40:8takriban 1491 KK

    Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua.

  19. Kutoka 40:9takriban 1491 KK

    “Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu.

  20. Kutoka 40:10takriban 1491 KK

    Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana.

  21. Kutoka 40:11takriban 1491 KK

    Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu.

  22. Kutoka 40:12takriban 1491 KK

    “Mlete Aroni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji.

  23. Kutoka 40:13takriban 1491 KK

    Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani.

  24. Kutoka 40:14takriban 1491 KK

    Walete wanawe na uwavike makoti.

  25. Kutoka 40:15takriban 1491 KK

    Kisha watie mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutiwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.”