- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446 BC
Sinai & The Law
God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.
Mistari ya kipindi hiki
- Kutoka 40:16takriban 1491 KK
Mose akafanya kila kitu sawa kama vile Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:17takriban 1491 KK
Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili.
- Kutoka 40:18takriban 1491 KK
Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo.
- Kutoka 40:19takriban 1491 KK
Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:20takriban 1491 KK
Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake.
- Kutoka 40:21takriban 1491 KK
Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:22takriban 1491 KK
Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia
- Kutoka 40:23takriban 1491 KK
na kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:24takriban 1491 KK
Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu
- Kutoka 40:25takriban 1491 KK
na kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:26takriban 1491 KK
Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia
- Kutoka 40:27takriban 1491 KK
na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:28takriban 1491 KK
Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu.
- Kutoka 40:29takriban 1491 KK
Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Bwana alivyomwagiza.
- Kutoka 40:30takriban 1491 KK
Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia,
- Kutoka 40:31takriban 1491 KK
Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao.
- Kutoka 40:32takriban 1491 KK
Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose.
- Kutoka 40:33takriban 1491 KK
Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.
- Kutoka 40:34takriban 1491 KK
Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.
- Kutoka 40:35takriban 1491 KK
Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.
- Kutoka 40:36takriban 1491 KK
Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka;
- Kutoka 40:37takriban 1491 KK
lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka.
- Kutoka 40:38takriban 1491 KK
Kwa hiyo wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.
- Walawi 1:1takriban 1490 KK
Bwana akamwita Mose na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia,
- Walawi 1:2takriban 1490 KK
“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe au la kondoo na mbuzi.