Rukia maudhui

circa 1050–1010 BC

Samuel & King Saul

Israel demands a king; Samuel anoints Saul, whose disobedience leads to his rejection as God chooses a man after his own heart.

810 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. 1 Samweli 20:8takriban 1062 KK

    Lakini kwa habari yako wewe, mtende wema mtumishi wako, kwa sababu mmeingia kwenye agano pamoja naye mbele za Bwana. Kama nina hatia, basi niue wewe mwenyewe! Kwa nini unikabidhi kwa baba yako?”

  2. 1 Samweli 20:9takriban 1062 KK

    Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?”

  3. 1 Samweli 20:10takriban 1062 KK

    Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?”

  4. 1 Samweli 20:11takriban 1062 KK

    Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

  5. 1 Samweli 20:12takriban 1062 KK

    Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?

  6. 1 Samweli 20:13takriban 1062 KK

    Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

  7. 1 Samweli 20:14takriban 1062 KK

    Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa Bwana siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa,

  8. 1 Samweli 20:15takriban 1062 KK

    wala usiuondoe wema wako kwa jamaa yangu, hata kama ni wakati ule Bwana atakapokuwa amekatilia mbali kila adui wa Daudi kutoka kwenye uso wa dunia.”

  9. 1 Samweli 20:16takriban 1062 KK

    Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: “Bwana na awaangamize adui za Daudi.”

  10. 1 Samweli 20:17takriban 1062 KK

    Naye Yonathani akamtaka Daudi athibitishe tena kiapo chake cha kumpenda, kwa sababu Yonathani alimpenda Daudi kama nafsi yake mwenyewe.

  11. 1 Samweli 20:18takriban 1062 KK

    Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo. Itajulikana kwamba haupo kwa kuwa kiti chako kitakuwa hakina mtu.

  12. 1 Samweli 20:19takriban 1062 KK

    Kesho kutwa, inapokaribia jioni, nenda mahali pale ulipojificha wakati tatizo hili lilipoanza na usubiri karibu na jiwe la Ezeli.

  13. 1 Samweli 20:20takriban 1062 KK

    Nitapiga mishale mitatu kando yake, kama kwamba nilikwenda kulenga shabaha.

  14. 1 Samweli 20:21takriban 1062 KK

    Kisha nitamtuma mvulana na kumwambia, ‘Nenda ukaitafute mishale.’ Kama nikimwambia, ‘Tazama mishale iko upande huu wako! Uilete hapa,’ basi uje, kwa sababu hakika kama Bwana aishivyo, wewe ni salama, hakuna hatari.

  15. 1 Samweli 20:22takriban 1062 KK

    Lakini kama nikimwambia huyo mvulana, ‘Angalia, mishale iko mbele yako,’ basi inakupasa uondoke, kwa sababu Bwana amekuruhusu uende zako.

  16. 1 Samweli 20:23takriban 1062 KK

    Kuhusu yale tuliyozungumza wewe na mimi: kumbuka, Bwana ndiye shahidi kati yako wewe na mimi milele.”

  17. 1 Samweli 20:24takriban 1062 KK

    Basi Daudi akajificha shambani, na sikukuu ya Mwezi Mwandamo ilipowadia, mfalme akaketi ili ale.

  18. 1 Samweli 20:25takriban 1062 KK

    Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi.

  19. 1 Samweli 20:26takriban 1062 KK

    Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.”

  20. 1 Samweli 20:27takriban 1062 KK

    Lakini siku iliyofuata, siku ya pili ya mwezi, kiti cha Daudi kilikuwa wazi tena. Kisha Sauli akamwambia mwanawe Yonathani, “Kwa nini mwana wa Yese hajaja chakulani jana wala leo?”

  21. 1 Samweli 20:28takriban 1062 KK

    Yonathani akamjibu, “Daudi alinisihi sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu.

  22. 1 Samweli 20:29takriban 1062 KK

    Alisema, ‘Niruhusu niende, kwa sababu jamaa yetu wana dhabihu mjini, na ndugu yangu ameniagiza niwepo huko. Kama nimepata kibali mbele yako, niruhusu niende kuona ndugu zangu.’ Hii ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme.”

  23. 1 Samweli 20:30takriban 1062 KK

    Hasira ya Sauli ikawaka dhidi ya Yonathani na kumwambia, “Wewe mwana wa mwanamke mkaidi na mwasi! Je, sijui kuwa umekuwa upande wa mwana wa Yese kwa aibu yako mwenyewe na kwa aibu ya mama yako aliyekuzaa?

  24. 1 Samweli 20:31takriban 1062 KK

    Maadamu mwana wa Yese angali anaishi katika dunia hii wewe wala ufalme wako hautasimama. Sasa tuma aitwe umlete kwangu, kwa kuwa ni lazima afe!”

  25. 1 Samweli 20:32takriban 1062 KK

    Yonathani akamuuliza baba yake, “Kwa nini auawe? Kwani amefanya nini?”