circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Timotheo 6:18takriban 65 BK
Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali zao na wengine.
- 1 Timotheo 6:19takriban 65 BK
Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.
- 1 Timotheo 6:20takriban 65 BK
Timotheo, linda kile kilichowekwa amana kwako. Epuka majadiliano yasiyo ya utauwa na mabishano ambayo kwa uongo huitwa elimu,
- 1 Timotheo 6:21takriban 65 BK
ambayo wengine kwa kujidai kuwa nayo wameiacha imani. Neema iwe nanyi. Amen.
- 2 Timotheo 1:1takriban 66 BK
Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu.
- 2 Timotheo 1:2takriban 66 BK
Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa: Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
- 2 Timotheo 1:3takriban 66 BK
Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
- 2 Timotheo 1:4takriban 66 BK
Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha.
- 2 Timotheo 1:5takriban 66 BK
Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo.
- 2 Timotheo 1:6takriban 66 BK
Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu.
- 2 Timotheo 1:7takriban 66 BK
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
- 2 Timotheo 1:8takriban 66 BK
Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu,
- 2 Timotheo 1:9takriban 66 BK
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.
- 2 Timotheo 1:10takriban 66 BK
Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili.
- 2 Timotheo 1:11takriban 66 BK
Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii.
- 2 Timotheo 1:12takriban 66 BK
Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.
- 2 Timotheo 1:13takriban 66 BK
Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu.
- 2 Timotheo 1:14takriban 66 BK
Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.
- 2 Timotheo 1:15takriban 66 BK
Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.
- 2 Timotheo 1:16takriban 66 BK
Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu.
- 2 Timotheo 1:17takriban 66 BK
Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata.
- 2 Timotheo 1:18takriban 66 BK
Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.
- 2 Timotheo 2:1takriban 66 BK
Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu.
- 2 Timotheo 2:2takriban 66 BK
Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile.
- 2 Timotheo 2:3takriban 66 BK
Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu.