Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Timotheo 5:18takriban 65 BK

    Kwa maana Maandiko husema, “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka,” tena, “Mfanyakazi anastahili mshahara wake.”

  2. 1 Timotheo 5:19takriban 65 BK

    Usiendekeze mashtaka dhidi ya mzee isipokuwa yawe yameletwa na mashahidi wawili au watatu.

  3. 1 Timotheo 5:20takriban 65 BK

    Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa.

  4. 1 Timotheo 5:21takriban 65 BK

    Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.

  5. 1 Timotheo 5:22takriban 65 BK

    Usiwe na haraka kumwekea mtu mikono wala usishiriki dhambi za watu wengine. Jilinde nafsi yako uwe safi.

  6. 1 Timotheo 5:23takriban 65 BK

    Acha kunywa maji peke yake, tumia divai kidogo kwa sababu ya tumbo lako na maumivu yako ya mara kwa mara.

  7. 1 Timotheo 5:24takriban 65 BK

    Dhambi za watu wengine ni dhahiri nazo zinawatangulia kwenda hukumuni; na dhambi za watu wengine zinawafuata nyuma yao.

  8. 1 Timotheo 5:25takriban 65 BK

    Vivyo hivyo, matendo mema yako dhahiri, na hata yale ambayo si mema hayawezi kufichika.

  9. 1 Timotheo 6:1takriban 65 BK

    Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.

  10. 1 Timotheo 6:2takriban 65 BK

    Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao ni waaminio, ambao ni wapenzi wao. Fundisha mambo haya na uwahimize kuyafuata.

  11. 1 Timotheo 6:3takriban 65 BK

    Ikiwa mtu yeyote atafundisha mafundisho mapotovu wala hakubaliani na mafundisho manyofu ya Bwana wetu Yesu Kristo na yale ya utauwa,

  12. 1 Timotheo 6:4takriban 65 BK

    huyo amejivuna wala hajui kitu chochote. Yeye amejaa tamaa ya mabishano na ugomvi kuhusu maneno ambavyo matokeo yake ni wivu na mapigano, maneno ya ukorofi, shuku mbaya,

  13. 1 Timotheo 6:5takriban 65 BK

    na kuzozana kusikokoma kati ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, na ambao hudhani kwamba utauwa ni njia ya kupata faida.

  14. 1 Timotheo 6:6takriban 65 BK

    Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa.

  15. 1 Timotheo 6:7takriban 65 BK

    Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu.

  16. 1 Timotheo 6:8takriban 65 BK

    Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo.

  17. 1 Timotheo 6:9takriban 65 BK

    Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka huanguka kwenye majaribu, na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi.

  18. 1 Timotheo 6:10takriban 65 BK

    Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

  19. 1 Timotheo 6:11takriban 65 BK

    Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

  20. 1 Timotheo 6:12takriban 65 BK

    Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi.

  21. 1 Timotheo 6:13takriban 65 BK

    Nakuagiza mbele za Mungu avipaye vitu vyote uhai, na mbele za Kristo Yesu ambaye alipokuwa anashuhudia mbele ya Pontio Pilato alikiri ukiri mzuri,

  22. 1 Timotheo 6:14takriban 65 BK

    uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,

  23. 1 Timotheo 6:15takriban 65 BK

    ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe: yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana,

  24. 1 Timotheo 6:16takriban 65 BK

    yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.

  25. 1 Timotheo 6:17takriban 65 BK

    Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.