Rukia maudhui

circa 1406–1380 BC

Conquest of Canaan

Joshua leads Israel across the Jordan into the promised land, defeating the Canaanite kingdoms one by one.

658 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Yoshua 15:50takriban 1443 KK

    Anabu, Eshtemoa, Animu,

  2. Yoshua 15:51takriban 1443 KK

    Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.

  3. Yoshua 15:52takriban 1443 KK

    Arabu, Duma, Ashani,

  4. Yoshua 15:53takriban 1443 KK

    Yanimu, Beth-Tapua, Afeka,

  5. Yoshua 15:54takriban 1443 KK

    Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.

  6. Yoshua 15:55takriban 1443 KK

    Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,

  7. Yoshua 15:56takriban 1443 KK

    Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,

  8. Yoshua 15:57takriban 1443 KK

    Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.

  9. Yoshua 15:58takriban 1443 KK

    Halhuli, Beth-Suri, Gedori,

  10. Yoshua 15:59takriban 1443 KK

    Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.

  11. Yoshua 15:60takriban 1443 KK

    Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.

  12. Yoshua 15:61takriban 1443 KK

    Huko jangwani: Beth-Araba, Midini, Sekaka,

  13. Yoshua 15:62takriban 1443 KK

    Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.

  14. Yoshua 15:63takriban 1443 KK

    Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

  15. Yoshua 16:1takriban 1443 KK

    Mgawanyo wa Yosefu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli.

  16. Yoshua 16:2takriban 1443 KK

    Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia eneo la Waariki huko Atarothi,

  17. Yoshua 16:3takriban 1443 KK

    ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.

  18. Yoshua 16:4takriban 1443 KK

    Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yosefu, walipokea urithi wao.

  19. Yoshua 16:5takriban 1443 KK

    Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,

  20. Yoshua 16:6takriban 1443 KK

    na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmeta upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki hadi Taanath-Shilo, ukiupita hadi Yanoa upande wa mashariki.

  21. Yoshua 16:7takriban 1443 KK

    Kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani.

  22. Yoshua 16:8takriban 1443 KK

    Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.

  23. Yoshua 16:9takriban 1443 KK

    Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.

  24. Yoshua 16:10takriban 1443 KK

    Hawakuwatoa Wakanaani waishio Gezeri; mpaka leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu lakini wanatakiwa kufanya kazi ngumu za kulazimishwa.

  25. Yoshua 17:1takriban 1443 KK

    Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu.