Rukia maudhui

Israel

1,007 mistari · 20 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Jacob

Mistari inayomtaja Israel

Chuja kwa kitabu
  1. kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake.

  2. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu. Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!

  3. hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo.

  4. Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.

  5. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.

  6. Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

  7. Nao husema, “Bwana haoni, Mungu wa Yakobo hafahamu.”

  8. Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa.

  9. Alijulisha Mose njia zake, na wana wa Israeli matendo yake.

  10. enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

  11. Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:

  12. Kisha Israeli akaingia Misri, Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.

  13. Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

  14. Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo,

  15. Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:

  16. mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

  17. Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani.

  18. Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,

  19. Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

  20. Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.

  21. Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

  22. Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.

  23. Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.

  24. Nitamngojea Bwana, ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake. Nitaliweka tumaini langu kwake.

  25. Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli.