Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Women

304 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mfalme na wakuu wake walipendezwa na shauri hili, hivyo basi mfalme akafanya kama Memukani alivyopendekeza.

  2. Alipeleka barua katika sehemu zote za ufalme wake, kwa kila jimbo kwa maandishi yake mwenyewe na kwa kila watu katika lugha yao wenyewe, akitangaza kwa msemo wa kila watu kwamba inampasa kila mwanaume kuwa mtawala wa nyumba yake mwenyewe.

  3. Msichana huyu alimpendeza na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya uzuri na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka jumba la kifalme, na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake.

  4. Kila siku Mordekai alikuwa akitembeatembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake kujua Esta alivyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.

  5. Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

  6. yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.

  7. Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke,

  8. kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.

  9. Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua?

  10. Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua?

  11. Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.

  12. Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

  13. Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe;

  14. kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.

  15. Hatakubali fidia yoyote; atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.

  16. Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha.

  17. Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili.

  18. Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke

  19. wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.

  20. Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.

  21. (Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;

  22. mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)

  23. Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:

  24. “Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.

  25. Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!