Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Women

304 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.

  2. Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.

  3. Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!

  4. Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.

  5. Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

  6. Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.

  7. Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,

  8. mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.

  9. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.

  10. Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.

  11. Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.

  12. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

  13. Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu.

  14. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.

  15. Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

  16. Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

  17. Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.

  18. Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

  19. Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

  20. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

  21. Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.

  22. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

  23. Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua.

  24. Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.

  25. “Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia: