Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Unbelief

208 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea.

  2. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’

  3. Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu.

  4. Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni?

  5. Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

  6. Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake.

  7. Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

  8. Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”

  9. wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye.

  10. Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.

  11. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.

  12. Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?

  13. Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu.

  14. Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”

  15. Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini.

  16. Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?”

  17. Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananungʼunika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi?

  18. Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?

  19. Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti.

  20. Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.

  21. Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.”

  22. (Hapa alikuwa anasema juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Yesu.)

  23. Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.

  24. Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”

  25. Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini!