Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Reproof

165 mistari · 70 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

  2. Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima.

  3. Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.

  4. Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.

  5. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

  6. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  7. Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu.

  8. Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. Lakini nitakukemea na kuweka mashtaka mbele yako.

  9. Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

  10. Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

  11. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.

  12. Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

  13. Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. Kichwa changu hakitalikataa. Hata hivyo, maombi yangu daima ni kinyume cha watenda mabaya,

  14. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  15. Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

  16. Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

  17. “Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.

  18. Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.

  19. Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.

  20. Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.

  21. Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.

  22. Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.

  23. Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa.

  24. Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima.

  25. Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima.