Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Reproof: God gives reproof to his own children

8 mistari · 70 vipengele

Mistari kuhusu God gives reproof to his own children

  1. Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu.

  2. “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

  3. Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

  4. Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

  5. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.

  6. Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

  7. kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, na humwadhibu kila mmoja anayemkubali kuwa mwana.”

  8. Vumilieni taabu kwa ajili ya kufunzwa adabu. Mungu anawatendea ninyi kama watoto wake, kwa maana ni mtoto yupi asiyeadibishwa na mzazi wake?