Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Reproof: The Scriptures are profitable for

6 mistari · 70 vipengele

Mistari kuhusu The Scriptures are profitable for

  1. Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima.

  2. Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.

  3. Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.

  4. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

  5. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  6. Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,