Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Red Sea

47 mistari · 6 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu.

  2. “Uliona mateso ya baba zetu huko Misri, ukasikia kilio chao huko Bahari ya Shamu.

  3. Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo.

  4. Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita katikati yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi.

  5. Alifanya bahari kuwa nchi kavu, wakapita kati ya maji kwa miguu, njooni, tumshangilie.

  6. Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta.

  7. Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao.

  8. Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

  9. Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.

  10. Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.

  11. Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.

  12. Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja.

  13. miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.

  14. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  15. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.

  16. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  17. Hili ndilo asemalo Bwana, yeye aliyefanya njia baharini, mahali pa kupita kwenye maji mengi,

  18. aliyeyakokota magari ya vita na farasi, jeshi pamoja na askari wa msaada, nao wakalala huko, wala hawatainuka tena kamwe, wakakomeshwa, na wakazimika kama utambi:

  19. Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.

  20. Ndugu zangu, sitaki mkose kufahamu ukweli huu kwamba baba zetu walikuwa wote chini ya wingu na kwamba wote walipita katikati ya bahari.

  21. Wote wakabatizwa kuwa wa Mose ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari.

  22. Kwa imani, watu walivuka Bahari ya Shamu kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, walitoswa ndani ya maji.