Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Faith

543 mistari · 124 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.

  2. Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.

  3. Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”

  4. Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

  5. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.

  6. Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao,

  7. ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

  8. Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake.

  9. Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

  10. Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

  11. Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,

  12. basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, hakuna maafa yataikaribia hema yako.

  13. Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake, hatauacha urithi wake.

  14. Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki, wote walio na mioyo minyofu wataifuata.

  15. Kama Bwana asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

  16. Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.

  17. Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

  18. Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?

  19. Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

  20. Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.

  21. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

  22. Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

  23. Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni,

  24. atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa.

  25. Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu.